WALIOHUDHURIA
- Wakati Kabaka
- Adam Millinga
- Godlisten Anderson
- Freddy Kyara
- Davis Kawa
- Elizabeth Samson
- Gemima Mabula
- Willehadi Akaro
Kikao kilianza saa 9 :45 alasiri na
kufunguliwa na Mwenyekiti, Ndugu Wakati Kabaka.
AJENDA
- Usajili wa kikundi
- Taarifa ya fedha
- Taarifa ya matukio yaliyopita
- Katiba
- Mengineyo
1.
USAJILI WA
KIKUNDI
Nyaraka zote muhimu zinazohitajika
kwa ajili ya uandikishwaji ziko tayari, imebaki kupata barua toka kwa ofisi ya
Mkuu wa Wilaya/Mkoa kwa uthibitisho
2.
TAARIFA YA
FEDHA
Wajumbe walisomewa taarifa ya
makusanyo na matumizi ya fedha zilizokusanywa tokea mwanzo wa kikundi.
Pia wajumbe walitoa wazo la
kupanga upya tarehe ya kuanza kukusanya michango ya mwezi, ili kuwapa wajumbe
ambao walichelewa kujiunga fursa ya kuwa na mzigo mdogo wa madeni ili kuweza
kukamilisha jumla ya michango yote ambayo angetakiwa awe ametoa. Hivyo basi
tarehe ya mwanzo iliamuliwa iwe ni mwezi wa kwanza mwaka 2013.(Januari, 2013.
3.
TAARIFA YA
MATUKIO YALIYOTOKEA
Kulikuwa na baadhi ya matukio kwa
wanamapambano 1999 na kama marafiki wajumbe waliwatembelea ili kuwajulia hali.
Jumla ya michango ilikuwa ni shilingi 440,000/ - na iligawanywa kwa wajumbe
waliotembelewa kama pole/faraja.
a)
Rabiel (Jimmy) Masue kupata ajali
alipokuwa safarini kuelekea Mwanza. Kwa sasa anaelendelea vizuri na bado
amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, taasisi ya MOI, PRIVATE WARD – G.
b)
Celina Fernandes aliyefanyiwa
operation. Kwa sasa anaendelea vizuri, yeye na mtoto na yupo nyumbani.
c)
Cecilia Simba aliyefiwa na baba
mlezi.
Wajumbe wamepanga pia kwenda
kuwatembelea Erasto Mavika na Balaja Mbogoma, ambao wamebahatika kupata watoto
pia.
4.
KATIBA
Wajumbe wameona kuna umuhimu wa
kuipitia katiba ya kikundi upya na kufanya marekebisho wa baadhi ya sehemu
zinazotakiwa.
5.
MENGINEYO
Kulikuwa na taarifa za matukio
mbalimbali kama ifuatavyo:
a) Send off ya Mwanazali Mmevela
inayotarajiwa kuwa tarehe 10/09/2013
b) Ndoa ya Wakati Kabaka
inayotarajiwa kuwa tarehe 01/11/2013
Adam Millinga aliombwa na Wakati
kukusanya/kupokea michango ya wanamapambano.
c) Ndoa ya ya Kudra Mbarouk
inayotarajiwa kuwa tarehe 24/10/2013
Pia wajumbe walipanga kufanya
“barbecue day” siku ya jumamosi ya mwisho ya mwezi wa tisa (9) na kwa makadirio
yaliyofanywa, kila mjumbe atatakiwa kutoa shilingi elfu ishirini (20,000/-) .
Eneo la tukio litatangazwa baadaye.
Kikao
kilifungwa na Mwenyekiti saa 11:00 jioni. Kikao kijacho kitafanyika tarehe
29/09/2013.
No comments:
Post a Comment