Pages

Tuesday, December 4, 2012

KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA WANAMAPAMBANO KILICHOFANYIKA TAREHE 02/12/2012, BULL’S PARK SURVEY
KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA WANAMAPAMBANO KILICHOFANYIKA TAREHE 02/12/2012, BULL’S PARK SURVEY
WALIOHUDHURIA
  1. Wakati Kabaka
  2. Harieth Shoo
  3. Adam Millinga
  4. Hatibu Simba
  5. Godlisten Anderson
  6. Cesilia Simba
  7. Elizabeth Samson
  8. Mei Maneno
Kikao kilianza saa 10:00 jioni na kufunguliwa na Mwenyekiti, ndugu Wakati Kabaka.
AJENDA
  1. Usajili wa kikundi
  2. Taarifa ya fedha
  3. Ufung
    uzi/uzinduzi wa blog ya kikundi
  4. Get together
  5. Mchango wa hisani
  6. Mengineyo
  1.      USAJILI WA KIKUNDI
Idadi ya sahihi zinazotakiwa kufikiwa ili kuweza kupeleka maombi ya usajili wizarani (mambo ya ndani) haikutimia, hivyo basi wahusika waliomba waongezewe muda wa kukusanya sahihi na kupeleka maombi hayo. Waliokabidhiwa jukumu hilo ni Wakati Kabaka na Hatibu Simba
  2.      TAARIFA YA FEDHA
Muweka Hazina,ndugu Frederick Kyara aliomba udhuru kutokana na kuuuguza, hivyo basi taarifa ya fedha haikuweza kusomwa.
  3.      UFUNGZI/UZINDUZI WA BLOG YA KIKUNDI
Blog ya kikundi imeweza kutengenezwa na inaweza kutembelewa kupitia anuani ya mapambanoprimary.blogspot.com. Kupitia hiyo, matangazo na habari mbalimbali zitaweza kupatikana na kuwafikia walio wengi. Kutokana na hilo, mawazo yalitolewa kuwa:
a)      Blog iweze kutumika katika kutangaza matangazo mbalimbali ya kibiashara, hasa katika kuinua biashara, kazi, habari za wanamapambano.
-katika hili, wanamapambano watakuwa na fursa ya kutangaza biashara zao bure kwa muda fulani (grace period) kabla ya kuanza kulipia ada ambayo ni ya chini na inayovumilika kama mchango kwa kikundi.
-kwa matangazo ya wasio wanamapambano(non-members) watakuwa na ada maalumu kwa mwezi au kwa mwaka ambayo moja kwa moja itaingia kwenye mfuko wa kikundi.
b)      Kwa wale wenye picha za matukio mbalimbali, wameombwa kuziwasilisha ili ziweze kuwekwa kama kumbukumbu katika blog. Jukumu la kuzikusanya na kuzipokea picha amepewa ndugu Godlisten Anderson.
  4.      GET TOGETHER
Katika njia mojawapo ya kuwakutanisha wanamapambano, mawazo mbalimbali yalitolewa kuhusu kufanya ‘get together’. Wazo lilitolewa kuifanya katika kisiwa cha Mbudya,kilichopo Bahari ya Hindi. Wanamapambano wameombwa kuendelea kutoa maoni yao katika hili, kuhusu eneo na tarehe muafaka ya kuifanya shughuli hii.
  5.      MCHANGO WA HISANI
  • Mawazo yalitolewa kuhusu wanamapambano kuchanga na kwenda kutembelea Shule ya Msingi Mapambano, iliamuliwa kuwa tarehe muafaka ya kufanya matembezi hayo ni siku ya Ijumaa tarehe 18,mwezi wa kwanza mwaka 2013. Hii ilitokana na umuhimu wa kuwapata wanafunzi, ambao ndio wahusika wakuu wataofaidika na msaada/mchango.
  • Ilikubaliwa kuwa kima cha chini kiwe ni shilingi elfu thelathini (30,000/-), na siku ya mwisho kuchanga itakuwa ni tarehe 11, mwezi wa kwanza mwaka 2013.
  • Vifaa vitakavyopewa vitagongwa muhuri, kama kumbukumbu ya ushirikiano wa wanamapambano.
  • Mawazo yamekaribishwa kuhusu hili hasa katika kutoa ushauri wa vifaa gani vinunuliwe na kukabidhiwa kwa wanafunzi
  6.      MENGINEYO
Taarifa za maandalizi ya harusi ziliwasilishwa, ambapo wanamapambano wanatarajia kufunga pingu za maisha, muda mfupi ujao, nao ni :
a)      Sauda Masoli anayetarajia kufanya send off tarehe 5 Januari, 2013
b)      Wakati Kabaka anayetarajia kufunga ndoa tarehe 22 Februari, 2013
c)      Emily Nkumbi  anayetarajia kufunga ndoa tarehe 23 Februari, 2013
Wanamapambano wameombwa kutoa ushirikiano wao katika kufanikisha haya matukio.

Kikao kilifungwa na Mwenyekiti saa 11:30 jioni. Kikao kijacho kitafanyika tarehe 06/01/2013.

No comments:

Post a Comment